Viwanja hivyo vitakuwa Libreville Franceville, vilivyotumika mwaka wa 2012,huku Port Gentil na Oyem
zikitarajiwa kukamilishwa katika kipindi cha miezi 14 ijayo kwa mujibu wa onyesho la shirikisho la soka la Gabon.
Gabon, inayopewa nafasi ya kushinda kinyang'anyiro hicho, iliandaa kwa pamoja na majirani zao Equatorial Guinea, fainali za mwaka 2012
| Timu ya Gabon |
Kamati ya shirikisho la vyama vya soka barani Afrika, Caf, itaendesha uteuzi huo katika mkutano wake wa mwaka utakaofanyika mjini Cairo,
Misri kuamua nani atakuwa mwenyeji wa fainali hizo.
Ghana iliandaa imewahi kuandaa fainali za mwaka 1963, 1978 na 2008 na iliandaa kwa pamoja na Nigeria fainali za
mwaka 2000 kama waandaji mbadala wakati Zimbabwe iliponyang'anywa haki ya kuandaa fainali hizo.
Algeria iliandaa fainali za mwaka 1990 wakati waliposhinda taji hilo pekee barani Afrika.
Caf pia inatarajiwa kupanga ratiba ya kufuzu kwa fainali hizo, ambayo itazishirikisha pia nchi za Morocco na Tunisia.
Morocco ilifungiwa kushiriki katika fainali mbili mfululizo za shirikisho la Caf baada ya kushindwa kuandaa fainali za mwaka 2015
lakini walishinda kesi hiyo baada ya kukata rufaa katika mahakama ya michezo, CAS.
Tunisia imeondolewa adhabu ya kutoshiriki michuano ya shirikisho hilo baada ya kuomba radhi kwa kulishutumu shirikisho hilo kwa upendeleo.
No comments:
Post a Comment