Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana
wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) imeingia kambini jijini Dar es
Salaam chini ya kocha mkuu Adolf Rishard kujiandaa na progamu ya vijana
kuwania kufuzu kwa fainali za U-17 mwaka 2017 nchini Madagascar.
Mwezi Februari 2016 timu hiyo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za mikoa ya Dodoma na Mwanza, kabla ya kuelekea tena katika ziara kwenye nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya mwezi Aprili 2016.
Mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana, Ayoub Nyenzi amesema kamati yake imeandaa programu maalumu ya kuwaanda vijana kwa ajili ya kuichezea timu ya Taifa U-17 mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment