Raia
wa Australia Andrew Chan (kushoto) na Myuran Sukumaran wanaosubiria
kuuawa kwa kupigwa risasi kesho asubuhi nchini Indonesia.
Dada
wa Sukuraman, Brintha, akisaidiwa na watu kuelekea bandarini wakati
akienda kumuaga kaka yake kwa mara ya mwisho kwenye Kisiwa
cha Nusakambangan.
Michael Chan (katikati mwenye tisheti ya kijani) ambaye ni kaka wa
Andrew Chan, akikatiza kwa wanahabari kuelekea bandarini tayari kwenda
kumuaga kaka yake.
Majeneza ya Chan na Sukuraman yakiwasili katika Kisiwa cha Nusakambangan.
Mama
mzazi wa Sukuraman, Raji (katikati), akilia kwa simanzi wakati
akiwasili katika bandari ya Wijaya Pura kuelekea Kisiwa cha
Nusakambangan kumuaga mwanaye.
Wanahabari wakiwazingira wanafamilia wa Chan na Sukumaran ili kupata picha za matukio.
Brintha Sukumaran ilibidi abebwe baada ya kuwasili katika gereza lililopo Kisiwa cha Nusakambangan.
VIGOGO wawili katika sakata la kutaka kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin kutoka nchini Indonesia, Andrew Chan na Myuran Sukumaran wanatarajia kuuawa kwa kupigwa risasi kesho Jumatano asubuhi.
Familia za vigogo hao jana zilitawaliwa na simanzi wakati zikiwaaga kwa mara ya mwisho wapendwa wao hao waliopo katika gereza moja kwenye Kisiwa cha Nusakambangan nchini Indonesia.
Majeneza ya Chan na Sukumaran tayari yamepelekwa katika kisiwa hicho kinachojulikana kwa jina maarufu la 'death island' likimaanisha kisiwa cha kifo.
Andrew Chan na Myuran Sukumaran walikuwa viongozi wa kundi la watu tisa walionaswa wakitaka kusafirisha kilo 8.3 za dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya zaidi ya bilioni 6, Aprili 17, 2005 huko Denpasar, Bali nchini Indonesia. Kundi hilo lilipewa jina la Bali Nine.
Kundi la Bali Nine lilikuwa likiwahusisha raia wa Australia tisa ambao ni Andrew Chan, Si Yi Chen, Michael Czugaj, Renae Lawrence, Tan Duc Thanh Nguyen, Matthew Norman, Scott Rush, Martin Stephens na Myuran Sukumaran.
Mwaka 2006 watuhumiwa saba kati ya tisa walihukumiwa kifungo cha maisha jela huku Andrew Chan na Myuran Sukumaran wakihukumiwa kuuwa kwa kupigwa risasi.
No comments:
Post a Comment