Polisi nchini Marekani wamesema kuwa watu tisa wameuawa katika shambulio
lililotekelezwa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki katika
mkahawa mmoja katika mji wa Waco.
Hata hivyo watu wengine 18 walipelekwa hospitali kupatiwa matibabu
kutokana shambulio hilo. Maofisa katika mji huo wanasema kuwa walibaini
mkusanyiko kati ya watu watano walioonekana kupanga jambo lisilo la
kawaida. Watu waliokuwa katika mkahawa huo walijificha katika chumba cha
majokofu katika harakati za kujiokoa kabla ya kusaidiwa na Polisi
kutoka katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment