Adebayor ametupia picha hii Facebook na kuahidi kutoa sehemu ya 2 ya stori ya kaka yake Rotimi.
SAKATA la straika wa Klabu ya Tottenham ya nchini Uingereza, Emmanuel
Adebayor na familia yake limechukua sura mpya ambapo staa huyo ameahidi
kutoa sehemu ya pili ya stori 'ubuyu' mwingine kuhusu kaka yake
mwingine aitwaye Rotimi Adebayor muda muafaka ukifika.
Adebayor ameahidi kutoa ubuyu huo ikiwa ni siku chache tangu aachie
waraka wa kwanza kupitia ukurasa wa Facebook uliokuwa ukielezea mambo
anayofanyiwa na familia yake mbali na fadhila nyingi alizowafanyia.
Katika waraka huo Adebayor alifunguka mambo mengi akielezea
anavyoibeba familia yake ambayo inaonyesha kutobebeka na badala yake
kumtupia lawama kuwa hana msaada wowote kwa familia hiyo.
Kusoma waraka wa kwanza
Baada ya waraka huo, dada yake aitwaye Lucia Adebayor aliibuka na
kukanusha taarifa hizo akidai ni uongo mtupu. Lucia aliandika hivi:
"Lipo
wapi gari ulilodai kumnunulia mama....si ulilichukua....Nyumba unayodai
ulimnunulia dada ni uongo mtupu... Simu unazodai Rotimi aliiba nao ni
uongo....fedha siyo kila kitu ooooo...sisi wanafamilia hatukutaki tena
fanya mambo yako na sisi tufanye yetu.... kuwa nazo leo si kigezo cha
kuwa nazo pia kesho Mwenyezi Mungu akusamehe...uliwafukuza wapwa wako
ndani ya nyumba yako saa 6 usiku....Alpha na Mallams zimekuharibia
maisha yako. Unamhitaji Mungu.... Mungu pekee ndiye anayeweza kuokoa
roho yako." aliandika Lucia ambaye Adebayor ndani ya waraka
wake wa mwanzo alimuelezea kuwa amekuwa akiwaambia watu kwamba baba yake
alimwambia ampeleke Ulaya japo yeye hakuona sababu ya kumleta dada yake
huyo Ulaya maana kila mtu yupo huko kwa sababu flani.
No comments:
Post a Comment