Pages

Thursday, 7 May 2015

BETHIDEI YAMRUDISHA KARRUECHE


Staa wa muziki wa Pop, nchini Marekani Christopher Maurice ‘Chris Brown.

STAA wa muziki wa Pop, nchini Marekani Christopher Maurice ‘Chris Brown’ hivi karibuni alisherehekea bethidei yake kwa kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Karrueche Tran.
Chanzo kinafunguka kuwa Chris alikuwa akitimiza miaka 26 akiwa kama baba wa mtoto mmoja, Royalty ambapo walianza kwa kuongozana na mrembo huyo katika onesho la ngumi kati ya Mayweather na Pacquiao.
Chris Brown akiwa na mpenzi wake Karrueche Tran.


“Chris alimpigia Karrueche simu sambamba na kumtumia meseji. Alikuwa na kila sababu ya kukutana naye kwanza Vegas kwenye onesho la ngumi na kweli baadaye alifanikiwa kufanya sherehe yake ya kuzaliwa kwa kutimiza ndoto ya kurudiana na Karrueche,” kilisema chanzo.
Chris na Karrueche walitengana kwa kile kilichoelezwa ni wivu wa kimapenzi ambapo bidada huyo aliamua kujitoa baada ya kugundua kuwa Chris alikuwa na mwanamke mwingine aitwaye Nia Amey-Guzman aliyezaa naye.

No comments:

Post a Comment