Bow Wow, amejitoa kwenye
Lebo ya Cash Money ambayo alidumu nayo kwa miaka mitano sasa.
Bow Wow aliyetesa na Kibao cha Let Me Hold You, ameamua kujitoa
kwenye lebo hiyo aliyosaini miaka mitano iliyopita kutokana na kutopata
mafanikio yoyote ya kimuziki mpaka sasa.
 |
| Bow Wow akiwa na aliyekuwa bosi wake Birdman. |
Alitumia muda wake kuposti video kwenye Mtandao wa Facebook akisema
anaondoka kwa amani na kuongeza kuwa hana tatizo na Cash Money wala
Birdman.
 |
| Rapa aliyeanza muziki tangu akiwa na miaka mitano, Bow Wow. |
Tangu ajiunge kwenye lebo hiyo, Bow Wow hakufanikiwa kuachia albamu
yoyote ya peke yake licha ya kurekodi ngoma kibao alizoishia
kuzisikiliza yeye tu, kitu ambacho kilimuuma zaidi.
Hata hivyo, imeripotiwa kuwa nyota huyo anarejea kufanya kazi chini
ya mastaa waliogundua kipaji chake tangu akiwa mtoto, Snoop Dogg na
Jermaine Dupri na hivi karibuni ataachia singo yake mpya.
No comments:
Post a Comment