Buhari anasema kuwa lengo lake ni kupambana ufisadi ambao umekita mizizi katika taifa hilo lenye watu wengie zaidi barabi Afrika. maelfu ya mashabiki na wafuasi wake walishangilia Jenerali huyo mtaafu alipokula kiapo cha kulinda nchi hiyo.
Viongozi kutoka mataifa mengi duniani wakiongozwa na waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John kerry , rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma miongoni mwa wengine wengi.
Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Nigeria kaskazini.
Anasemekana kuwa si m-kaishi, hakubali kushindwa.
Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan, Mkristo, anaye toka eneo la Niger Delta, kusini Nigeria, kwa mara ya pili, katika uchaguzi wa Machi. Unaonesha kuwa mchuano mkali.
Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na ukosefu wa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi. Kimataifa, Buhari pia anasemekana kuheshimiwa. Yajulikana kwamba ni yeye na marehemu Nelson Mandela tu ndio Wafrika binafsi waloalikwa na Ikulu ya White House, Marekani, kuhudhuria sherehe za kutawazwa Barack Obama.
Kampeni ya Jenerali Buhari, ilitilia mkazo mambo kadha, miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu, umeme na nishati, kilimo, elimu, afya, ardhi na usafiri, kuwezeshwa wanawake, usalama, na ajira. Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado unazusha masuala, je ni wa kijeshi au kidemomkrasi?
No comments:
Post a Comment