Uchina imesema imesikitishwa sana na
mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya raia wake sita na serikali ya
Marekani kwa madai ya ujasusi wa kiuchumi.
Maafisa wa mashtaka wa Marekani wanadai kuwa wachina hao waliiba taarifa nyeti kutoka kwa kampuni za kiteknolojia. Marekani zilizoko Silicon Valley ambako walikuwa wakifanya kazi ili kusaidia kampuni za Kichina kuwapiku kibiashara.Profesa Hao Zhang alitiwa mbaroni mjini Los Angeles lakini wengine watatu wako nchini Uchina.
Waandishi wa habari wanasema kuwa Uchina mara kwa mara hupuuzilia mbali madai ya ujasusi lakini inaonekana kuwa dhana hiyo inaendelea kukubalika nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment