Pages

Thursday, 28 May 2015

FIFA:Blatter aongoza kikao cha dharura

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter, ameongoza kikao cha dharura cha wanakamati wakuu wa shirikisho hilo huko Zurich Uswisi.
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter, ameongoza kikao cha dharura cha wanakamati wakuu wa shirikisho hilo huko Zurich Uswisi. Kikao hicho kinafuatia hatua ya kukamatwa kwa maafisa 7 wakuu na polisi huko Zurich Uswisi kwa tuhuma za ufisadi. Blatter anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu uongozi wa FIFA. Hata hivyo FIFA inasema kuwa kura za kumchagua rais mpya zilizoratibiwa kufanyika kesho zitaendelea mbele.

No comments:

Post a Comment