Wapiganaji wa kundi la Islamic State
wamekiri kwamba ndio waliotekeleza shambulizi katika shindano la
vibonzo vya kumkejeli mtume Muhammad (s.a.w.) katika jimbo la Texas
nchini Marekani.
Kundi hilo limesema kuwa wapiganaji wawili wa kundi hilo walitekeleza shambulizi hilo katika mkutano uliokuwa karibu na mji wa Dallas.
Taarifa ya habari ya Redio ya kundi hilo Al-Bayan imesema kuwa maonyesho hayo yalikuwa yakionyesha picha mbaya kumhusu mtume Muhammad.
Washukiwa wote wawili walipigwa risasi baada ya kufyatua risasi katika maonyesho hayo siku ya jumapili.
No comments:
Post a Comment