Pages

Sunday, 3 May 2015

IS yawaua raia 300 wa Yazidi nchini Iraq

Maafisa nchini Iraq wanasema kuwa wanamgambo wa islamic state wamewaua mamia ya watu wa yazidi waliokuwa wakiwazuilia eneo lililo kaskazini mwa nchi.
Raia wa Yazidi
Makamu wa rais nchini Iraq Osama al-Nujifi ameyalaani mauaji hayo akiyataja kuwa ya kikatili.

Taarifa zilisema kuwa hadi watu 300 waliuawa kwenye wilaya moja iliyo magharibi mwa mji wa Mosul siku ya ijumaa.


Wanamgambo wa islamic state walithibiti maeneo yaliyo kaskazini mwa Iraq kwa karibu mwaka mmoja uliopita ambapo waliwaua na kuwashika mateka maelfu ya watu wa Yazidi wakiwaita makafiri.

No comments:

Post a Comment