Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki-moon ameelezea tahadhari yake kuhusiana na hatari ya raia kuendelea
kupigana, Nchini Yemen.
Anasema kuwa zaidi ya watu elfu moja mia
tano wameuwawa na wengine laki tatu wametoroka makazi yao, katika
kipindi cha majuma sita yaliyopita, Mashambulizi katika majumba ya raia zikiwemo hosptali na maghala ya vifaa vya misaa ya kibinadamu yamekuwa yakiendelea.
Kumekuwa na taarifa watu wenye silaha wamekuwa wakiwateka raia katika mitaa ya Aden. Shirika
la Umoja wa mataifa la misaada ya chakula limesema halina jinsi zaidi
ya kusitisha mipango yake ya kusambaza misaada kutoka na tatizo la
mafuta.
Kwa sasa mapigano makali yanaendelea katika mipaka ya eneo la Yemen na Saudia Arabia. |
No comments:
Post a Comment