Ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya serehe hizo.
Katikati ni, Philipe Roisse kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UNESCO) akisalimiana na viongozi wengine.
Meza kuu iliyoandaliwa.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Shivji (katikati)
akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa nje ya ukumbi kabla ya kuanza
mkutano huo.
TANZANIA kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wameanza maadhimisho ya Wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika na kuzindua mradi wa nyaraka za urithi wa Tanzania.
Mwandishi wetu leo amefika katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kukuta maandalizi ya maadhimisho hayo yakiwa yamepamba moto huku baadhi ya viongozi na wageni waalikwa wakianza kuingia kwa ajili ya maadhimisho hayo.
Maadhimisho hayo yaliyoanza leo Mei 25, yanatarajiwa kumalizika Mei 29, mwaka huu. Lengo la maadhimisho hayo kwa ajili ya kudumisha kumbukumbu za ukombozi wa Bara la Afrika na ushiriki wa Tanzania kama mwenyekiti wa iliyokuwa kamati ya nchi za mstari wa mbele katika kupigania uhuru Kusini mwa Bara la Afrika.
STORI/PICHA: DENIS MTIMA/GPL
No comments:
Post a Comment