Man City yaichabanga Swansea 4-2
 |
| Yaya Toure |
Matokeo ya Mechi mbili za ligi kuu ya England zilizochezwa hapo jana,Manchester City iliwachabanga Swansea mabao 4-2. Ni Wilfried Bony
ambaye mnamo dakika ya 90 lililopigilia msumali wa moto kwa Swansea
baada ya kufunga bao la nne. Lakini Yaya Toure yeye alizifumania nyavu
mara mbili dakika 21 na 74. James Milner naye akifunga mnamo dakika ya
36.
Huku katika mechi ya pili Arsenal wakitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya
Man united,ambapo kwa matokeo hayo sasa Arsenal wanaendelea kujiimarisha
katika nafasi ya tatu. Leo West Brom watakipiga na Chelsea katika dimba
la The Hawthons.
No comments:
Post a Comment