Pages

Friday, 15 May 2015

MAPINDUZI YAFELI BURUNDI

Mnamo 13 mwezi May jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa. Lakini msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.
Maandamano  nchini Burundi dhidi ya rais Nkurunziza
Rais Nkurunziza alidaiwa kurudi nchini Burundi kutoka Tanzania ,lakini imethibitishwa kuwa leo, alishindwa kufanya hivyo na kwamba yungali nchini Tanzania.

Majenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wamekamatwa.
Hatahivyo kiongozi wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare ametoroka na anasakwa kulingana na msemaji wa rais.
Awali Jenerali Niyombare alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na wafuasi wake watajisalimisha akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa amerudi nchini Burund na kwamba anatarajiwa kulihutubia taifa.

No comments:

Post a Comment