Mchezaji kandanda ameahidi kulipia hasara iliyosababishwa na shabiki wake alipofunga bao.
Shabiki
huyo sugu Ross Morgan, 25, alikuwa akitizama mechi kati ya Ipswich na
Norwich jumamosi iliyopita wakati huo timu yake ikiwa nyuma kwa bao
moja.Hata hivyo anasema alishikwa na wazimu akaruka juu na kupiga ngumi dari ya nyumba yake ikatoboka baada ya Paul Anderson kufunga bao la kusawazisha.
Morgan aliipiga picha shimo hilo na akaiweka kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter.
Mashabiki wenza waliisambaza na ikamfikia Anderson ambaye ilimgusa na akajitolea kugharamia hasara aliyosababisha.
Anderson alijitolea kufidia gharama ya ufundi ilikuirejesha nyumba yake katika hali nzuri.
Mchezaji huyo wa Ipswich aliwatamausha mashabiki waliokuwa wakifuatilia mazungumzo yao kwa ukarimu wake.
Morgan, aliachwa kinywa wazi na ukarimu wa Anderson.
Kwa sasa shabiki huyo sugu anapania kutizama mechi ya marudiano kati ya Ipswich na Norwich katika uwanja wa Wembley siku ya jumamosi.
No comments:
Post a Comment