MAMLAKA YA Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) umetoa ufafanuzi juu ya kanuni ya uwianishaji wa mafao kipengele cha 13 ambacho kimekuwa kikilalamikiwa na wanachama wa mfuko huo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji, Sarah Kibonde Msika, alipokuwa akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es Salaam ambapo alisema kipengele hicho cha 13 kimekuwa kikilalamikiwa na wanachama wa mfuko wa hifadhi ya jamii kwa kutokielewa.
“Malalamiko mengi kutoka kwa wanachama wetu tumekuwa tukiyapokea kutokana na kipengele hicho, lakini kwa tafsiri ya mwanachama anayestafu kwa hiari atapunguziwa asilimia 0.3 kwa mwezi ambayo nia sawa na asilimia 3.6 kwa mwaka hadi pale atakapofika umri wake wa kustaafu wa miaka 60,” alisema Kibonde.
Aidha aliongeza kuwa pamoja na punguzo la asilimia 0.3 bado wastaafu wa hiari wanamzidi yule aliyestaafu akiwa na miaka 60 kwa asilimia 10, bila punguzo hilo tofauti na anayestaafu kwa hiari akiwa na miaka 55 ikiwa na tofauti ya asilimia 28 kwa wenzake.
NA DENIS MTIMA/GPL
No comments:
Post a Comment