Kauli hii ni msumari katika kidonda cha Morsi ambaye alikuwa tayari anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kuamrisha kukamatwa kwa waandamanaji waliopinga utawala wake.
Kufuatia uamuzi huo wa kifo , sasa kauli nzima na ruhusa itapatikana tu baada ya uamuzi kutumwa kwa kadhi mkuu nchini humo ambaye sasa ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho iwapo Morsi ataonja mauti au la .
Sheria za nchi hiyo hata hivyo zinamruhusu Morsi kukata rufaa licha ya uamuzi wa kadhi mkuu.
Morsi na wafuasi wake wamekuwa wakishikilia kukutu kuwa mashtaka dhidi yake yamechochewa na uhasma wa kisiasa baina yake na uongozi ulioko sasa.
Morsi amekataa katakata uhalali wa mahakama iliopo sasa.
Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru.
Hata hivyo utawala wake ulikumbwa na wimbi la maandamano baada ya kujilimbikizia madaraka akiwa amehudumu kwa mwaka mmoja tu ya kuwa afisini.
No comments:
Post a Comment