ADRIANNE LEWIS mwenye umri wa miaka 18 kutoka Michigan anafukuzia rekodi ya dunia kwa kuwa mtu mwenye ulimi mrefu kuliko wote.
Adrianne mwenye ulimi wa inchi nne anataka kuvunja rekodi inayoshikiliwa na Nick Stoeberl mwenye ulimi wa inchi 3.9. Dada huyo ana uwezo wa kugusa pua yake, kidevu chake, jicho na nyusi zake kwa kutumia ulimi huo. Adrianne ana chaneli yake katika mtandao wa YouTube ambapo anaweka video zake zinazoonyesha maajabu anayoweza kuyafanya kwa kutumia ulimi wake.
Adrianne Lewis akionyesha ulimi wake.
Adrianne mwenyewe anasema:'Nahisi kama nimerithi hali hii maana mama yangu, bibi na babu wote walikuwa na ndimi ndefu.
Nick Stoeberl.
Adrianne akiwa na mpenzi wake wakila ice cream.
No comments:
Post a Comment