Mke wa aliyekuwa nahodha wa kikosi
cha Manchester United pamoja na timu ya Uingereza Rio Ferdinand
amefariki kutokana na saratani. Mlinzi huyo wa kilabu ya QPR
mwenye umri wa miaka 36 alitoa taarifa akisema mkewe mpendwa Rebecca
Ellison aliaga dunia katika hospitali moja ya London.
Rio Ferdinand na marehemu mkewe
Marehemu Elison mwenye umri wa miaka 34 aliyeoana na Ferdinand mwaka 2009 alikuwa akiugua saratani ya titi.
Amewaacha watoto watatu.katika taarifa hiyo Ferdinand amesema kuwa mkewe alifariki ijumaa usiku.
''Rebecca,mkewe
wangu alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi na saratani katika
hospitali ya Royal Marsden mjini London'',alisema mchezaji huyo wa soka.
No comments:
Post a Comment