Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi
nchini Guinea ,Moussa Dadis Camara ametangaza kwamba atawania urais wa
taifa hilo baadaye mwaka huu.
Moussa Dadis Camara
Bwana Camara amekuwa akiishi mafichoni nchini Burkina Fasso baada ya kujeruhiwa katika jaribio la kumuua mwaka 2009.
Wakati
wa uongozi wake ,takriban watu 160 waliuawa baada ya vikosi vya
serikali kuwapiga risasi waandamanaji katika uwanja wa michezo wa mji
mkuu wa Conakry.
Wiki iliopita wafuasi wa bwana Camara walifanya maandamano wakimtaka arudi nchini humo.
No comments:
Post a Comment