Muuguzi mmoja amehukumiwa kwa makosa
ya kuwaua wagonjwa wake wawili na kuwapa wengine 20 sumu katika
hospitali ya Greater Manchester.
| Muuguzi |
Chua, mwenye umri wa miaka 49, aliondolewa kosa jingine la tatu la mauaji lakini akahukumiwa makosa mengine mengi dhidi ya wagonjwa wake kukiwemo mmoja ambapo mgonjwa alijeruhiwa ubongo wake.
Chua ambaye hakupatikana na kosa la kumuua Arnold Lancaster, mwenye umri wa miaka 81, lakini akapatikana na hatia ya kumwekea sumu kwenye dawa hakuonyesha hisia zo zote wake hukumu hiyo ilipokuwa ikitolewa. Atatangaziwa kifungo chake Jumanne.
Wagonjwa hao waliwekewa sumu kati ya Juni 2011 na Januari 2012.
No comments:
Post a Comment