Waziri mkuu wa Israeli Benjamin
Netanyahu ameelezea mshangao wake binafsi kwa mwanajeshi wa Israeli wa
asili ya Ethiopia ambaye alipigwa na polisi wa Israeli hali
iliyosababisha kutokea kwa maandamano.
Maandamano Israel
Bwana Netanyahu alimuambia Damas Fikadeh kuwa kitendo hicho hakikubaliki, na madabiliko yanahitaji kufanywa.
Waandamanaji Israel
Bwana Fikadeh alisema alitiwa moyo na matamshi yake waziri mkuu na ni
wakati wa kumaliza ghasia za ubaguzi dhidi ya Waisraeli wa asili ya
Ethiopia.
Wakati wa ghasi hizo za siku ya jumamosi usiku mjini Tel Aviv takriban watu 50 walijeruhiwa.
Wakati huohuo rais wa Israeli Reuven Rivlin amesema kuwa ni makosa
jinsi Israeli inavyowafanyia wayahudi wenye asili ya Ethiopia.
Akizungumza
baada ya maandamano yenye ghasia mjini Tel Aviv bwana Rivlin alisema
kuwa kidonda kilicho wazi kimeonekana nchini Israeli , lakini ghasia sio
suluhu.
Zaidi ya watu 50 walijeruhiwa siku ya Jumapili wakati polisi walitumia vituo machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji.
No comments:
Post a Comment