Pages

Sunday, 17 May 2015

Papa Francis amewatawaza Wapalestina 2

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewatawaza watawa wawili wa Kipalestina walioishi katika karne ya 19 wakati wa utawala wa Ottoman kuwa watakatifu.
Misa ya kuwatawaza watawa 2 wapalestina katika ukumbi wa st Peters Basilica huko Vatican
Watawa hao wawili walioishi miongoni mwa jamii ya wapalestina waarabu ,bi Marie Alphonsine Ghattas na Mariam Bawardy watakuwa miongoni mwa watakatifu watakao tawazwa hii leo katika ukumbi wa kanisa kubwa la papa Francis la St Peter's Square iliyoko Rome.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ni miongoni mwa mahujaji 2,000 wakristo waliofika katika makao makuu ya kanisa katoliki huko Vatican.
Hatua hii inatazamwa na wengi kama chambo cha kuwavutia wakristu katika maeneo ya mashariki ya kati ambapo wakristu wanahujumiwa na jamii.

No comments:

Post a Comment