Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ametangaza rasmi azma yake ya kugombea kwa awamu ya tatu katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo, licha ya kuendelea upinzani wa kila upande ndani na nje ya nchi hiyo wa kumtaka asifanye hivyo.
| Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza. |
Aidha rais huyo kijana aliahidi kuandaliwa haraka iwezekanavyo mazingira bora kwa ajili ya kufanyika uchaguzi ujao.
Tayari Tume Huru ya Uchaguzi nchini Burundi imemtaja Rais Pierre Nkurunziza kuwa mgombea wa kwanza kusajiliwa katika tume hiyo kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 26 Juni mwaka huu.
Hii ni katika hali ambayo maandamano ya kupinga kugombea tena Rais Nkurunzinza yangali yanaendelea nchini Burundi huku wimbi la wananchi wa Burundi wanaokilimbilia nchi jirani za Tanzania, Rwanda, na DRC nalo likizidi kuwa kubwa.
CHANZO: IRAN SWAHILI
No comments:
Post a Comment