Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza,
amepuuzia wito uliotolewa na nchi ya Marekani pamoja na umoja wa Ulaya
juu ya wito uliotolewa kuhusu uchaguzi uahirishwe. Rais Nkurunziza
amesema kwamba kuahirishwa kwa uchaguzi kutaliingiza taifa hilo
katika mgogoro mkubwa zaidi."unapoona asilimia tisini na tisa ya nchi
yote ina amani na usalama hii ina maana mazingira yanaruhusu uchaguzi
kufanyika .
Unaweza kusema kwamba uchaguzi usitishwe ikiwa watu wote wanazungumza lugha hiyo ya kusitishwa kwa uchaguzi ,na hiyo itakuwa na maana kwamba tutakuwa na serikali ya mpito.
Hatuwezi kukubaliana na wito huo hata kidogo hapa nchini Burundi,kwasababu kukubaliana na wito huo ni kukaribisha vurugu kubwa zaidi na matatizo makubwa zaidi mbeleni hasa tukiunda serikali ya mpito."
"kwa kawaida unapozungumzia juu ya suala la maandamano sio suala la kwenda kuua watu wala kuwashambulia polisi na hata kuchoma moto magari na kadhalika.
Ina maana kwamba yakitukia mabo kama hayo wakati wa maandamano basi hayo siyo maandamano,hiyo ni sawa na vita,ndiyo maana tunasikitika kutokana na vifo vilivyotokea wakati wa maandamano hayo lakini ni lazima tuwe na maamuzi ya kusitisha vurugu na hivyo basi kuwaruhusu watu kuingia kwenye harakati za uchaguzi."
No comments:
Post a Comment