Polisi wamelazimika kufyatua risasi
na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji waliokaribia makao ya rais
katika mji muu wa Bujumbura Burundi.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Maud Jullien amesema kuwa mamia ya waandamanaji walikuwa takriban kilomita moja kutoka kwa kasri ya rais ndipo wakavamiwa na maafisa wa usalama.
| Polisi wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji waliokaribia makao ya rais katika mji muu wa Bujumbura. |
Mkutano huo utakuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, aliyeuitisha baada ya ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Jumuiya hiyo, kwenda Bujumbura wiki iliyopita.
Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo,kusikiliza hoja za viongozi wenzake.
Viongozi hao wanatarajiwa kumshinikiza rais Nkurunzinza kuahirisha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi juni.
No comments:
Post a Comment