Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa
mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amesema ikiwa hatua ya kuondoa
majeshi ya Burundi itafanyika nchini Somalia itaathiri mapambano dhidi
ya wanamgambo wa Al Shabab.
mwanzoni mwa juma hili Marekani
ilitangaza kupunguza kiasi cha pesa inachotoa kwa majeshi ya Burundi
baada ya shutuma kuwa jeshi hilo limejihusisha katika vitendo vya
ukiukwaji wa haki za binaadam wakati wakizima vurugu zilizojitokeza
wakati jaribio la mapinduzi dhidi ya Serikali ya Rais Pierre Nkurunziza
liliposhindwa.AU nayo imesita kupeleka kundi jingine la wanajeshi wa Burundi nchini Somalia.Lakini Kay ameiambia BBC kuwa majeshi ya Umoja wa Afrika yanahitaji msaada kuweza kupambana na Al Shabaab.pia ametahadharisha kuongezeka kwa mahitaji ya kibinaadam nchini Somalia na kutoa wito wa jumuia ya kimataifa kuendelea kupeleka misaada nchini humo.
No comments:
Post a Comment