| Dismas Lyassa akizungumza na baadhi ya vijana katika kijiji cha Ihenga ambao wamekuwa wakifanya shughuli za kuvusha watu baada ya barabara kujaa maji. |
| Kutokana na magari kusitisha shughuli zao kutoka Ifakara kwenda vijijji mbalimbali vya Kilombero wananchi wengi wamekuwa wakitembea kwa miguu. |
Ndugu Wanahabari Uchaguzi Mkuu wenye lengo la kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais nchini unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini.
Nimekuwa
nikitembelea vijiji na kata mbalimbali za Wilaya ya Kilombero. Hivi
karibuni nilitembelea kata zote za wilaya, nilizungumza na wananchi,
wengi wao walinishauri kugombea Ubunge. Wananchi wanaamini kuwa kwa
pamoja tutaweza kuendeleza vema gurudumu la maendeleo kwa kasi zaidi.
Wananifahamu
kama mtoto wa masikini mwenzao niliyewahi kuzunguka mitaani kupiga
picha ili kuendesha maisha, mtoto wa masikini niliyewahi kuwa na ofisi
ya kusafisha viatu vya watu eneo la Ubungo Maziwa kwa mzee Mrisho ili
niweze kupata nauli ya kwenda shule wakati huo nasoma Chuo cha Elimu ya
Biashara (CBE).
Maisha
nayafahamu vizuri na nina uchungu nayo, natamani kushirikiana na
wananchi ili kuepukana na maisha duni. Katika maisha yangu kutokula au
wakati fulani kutembea kwa miguu kwenda chuo CBE na kurudi nyumbani
Ubungo Maziwa (nilikuwa naishi kwa dada), lilikuwa ni jambo la kawaida,
kwani maisha yalikuwa magumu mno.
Sauti ya wananchi wa Kilombero
Kilio
cha wananchi pamoja na mambo mengine ni kwamba wanahitaji kiongozi
kijana mwenye nguvu za kuongoza, kiongozi mwenye ujuzi wa namna ya
kuongoza na kutawala, kiongozi ambaye atakuwa bega kwa bega na wananchi
katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi. Kiongozi ambaye anajua
namna ya kuongoza, siyo namna ya kuhonga au kuwalisha yamini wapiga
kura, kwani wanachohitaji watu wa Kilombero ni maendeleo, siyo zaidi.
Hawahitaji kiongozi ambaye ni maarufu kwa kutembelea magari ya kifahari,
wanahitaji huduma za kijamii kama shule, hospitali na wao wenyewe
kusaidiwa namna ya kubuni miradi ya maendeleo.
Elimu
yangu ya juu ni Stashahada ya Uzamili katika Uongozi na Utawala
(Postgraduate Diploma in Leadership and Governance), kutoka Chuo cha
Utumishi wa Umma-Dar es Salaam niliyohitimu Aprili 22, 2014. Hata hivyo
nje ya elimu nimekuwa nikishughulika na masuala ya kijamii kupitia
kufanya mikutano ya ana kwa ana na jamii katika masuala ya ujasiriamali,
uchumba/ndoa na kadhalika.
Mojawapo
sababu za wananchi kuamini kwamba ninaweza kushirikiana nao kwa ufanisi
ni rekodi ambazo wananchi wenyewe wanazo juu yangu, kwani nimekuwa nao
karibu katika mambo mengi ya maendeleo ikiwamo kushirikiana nao moja kwa
moja au vikundi vyao hasa vya walemavu, kina mama, vijana
na kadhalika kama mshauri wao katika suala zima la namna ya kuviendesha
na kuwaunganisha na taasisi au watu wa kusaidiana nao.
Kwa
hivi sasa maeneo kadhaa ya Kilombero yanasaidiwa na mashirika
mbalimbali yakiwamo ya nje, baadhi yake ni kutokana na jitihada
zangu….nje ya uandishi wa habari, pia nimekuwa nikimiliki kampuni ya
kuwaunganisha watu na vyuo vya nje ya Global Source Watch (GSW), ambayo
imekuwa ikinipa fursa ya kujuana na watu wengi wa nje.
Nachukua fursa hii kutangaza rasmi kwamba nitachukua fomu ya kugombea Ubunge kutokana na kukidhi vigezo vyote ya kugombea nafasi hii kama ilivyojieleza katika Katiba ya Tanzania ibara ya 67.-(1) ambayo pamoja na mambo mengine inasema “Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
Nachukua fursa hii kutangaza rasmi kwamba nitachukua fomu ya kugombea Ubunge kutokana na kukidhi vigezo vyote ya kugombea nafasi hii kama ilivyojieleza katika Katiba ya Tanzania ibara ya 67.-(1) ambayo pamoja na mambo mengine inasema “Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
(a) ni
raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja,
na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
Mimi ni mzaliwa wa Kijiji
cha Mofu, wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Juni 26, 1976. Nimewahi
kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi
ikiwamo the Guardian Limited kama mwandishi wa kujitegemea, Uwazi kama
Mhariri, Leo ni Leo kama Mhariri wa Makala, Mwananchi kama Mwandishi wa
makala baadaye mhariri wa jarida la ndani ya biashara, the Media Project
(Marekani) kama mchangiaji nk.
Kwa sasa ni Kiongozi wa
Utafiti hapa nchini (National Lead Researcher) wa taasisi ya kimataifa
iitwayo Global Integrity yenye makazi yake Marekani, pia ni Mhariri
Mtendaji wa gazeti la Mwanahabari, lakini maamuzi haya ya kugombea
ubunge ni yangu binafsi hayana uhusiano wala hayataingiliana na sehemu
yoyote ninayofanyia kazi.
Nimewahi kutembea katika
nchi mbalimbali kwa lengo la kwa kusoma na kutembea, baadhi yake ni
Marekani, Kenya, Uganda, Dubai, Thailand, India.
OMBI KWA WASAMARIA WEMA
Napenda kuchukua fursa hii
pia kuwaomba wasamaria wema kuangalia namna ya kusaidiana na wananchi wa
Kilombero kwani wakati huu njia nyingi hazipitiki kwa sababu barabara
zimejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Magari yamekuwa
hayapitiki katika maeneo mengi ya Kilombero kwa sasa.
Kwa mfano sehemu kubwa ya barabara ya kutoka
Ifakara kwenda Mofu haipitiki, kiasi kwamba wagonjwa wamekuwa hawawezi
kubebwa kupelekwa Ifakara ambako ndiko pekee kuna hospitali ya Wilaya,
St Francis. Wapo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakibebwa kwa kutumia
baiskeli na hata pikipiki, jambo ambalo limekuwa gumu hasa kwa
wajawazito.
Magari
ya abiriia hasa Noah zilizokuwa zikifanya safari kutoka na kuingia
Ifakara kutoka vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Kilombero yamesitisha
safari kutokana na barabara kujaa maji. Yapo magari machache hasa ya
mizigo ambayo nayo yanafika baadhi ya vijijini kwa shida yakiwa yamebeba
mizigo na abiria hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi.
Mvua zimeathiri pia kilimo,
kwani mashamba mengi yamefurika maji, huku kukiwa na njaa kwa baadhi ya
wanavijiji. Hivyo nachukua fursa hii kuiomba Serikali kuchukua hatua za
haraka kusaidia wananchi wakiwamo wa vijiji vya Mofu, Ihenga, Mlimba,
Chisano, Chita, Mkula, Sanje, Uchindile na Utengule
No comments:
Post a Comment