Tetemeko kubwa la Ardhi limetikisa
tena Nepal ,takriban majuma mawili tu tangu tetemeko lingine kubwa zaidi
kusababisa vifo vya zaidi ya watu 8000.
Watafiti wanasema kuwa
kitovu cha tetemeko hilo lililikuwa katika mji wa Namche Bazar, karibu
zaidi na mlima mrefu zaidi duniani Mlima Everest.Tetemeko la awali lililotokea tarehe 25 Aprili , lilisajili vipimo vya 7.8.
Madhara ya tetemeko hili hayajabainika ila inasemekana kuwa lilitikisa mji mkuu wa India New Delhi, vilevile mji mkuu wa Bangladesh Dhaka.
Kulingana na walioshuhudia maelfu ya watu waliokuwa ndani ya majumba yao walitorokea sehemu za wazi hofu ikitanda kuwa madhara na vifo zaidi yatatokea.
''Jamani mungu atuokoe maanake tetemeko hili la hivi punde lilikuwa lakutisha zaidi.
lilikuwa kubwa mno ''anasema Prakash Shilpakar mkaazi wa Kathmandu
Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa sita adhuhuri saa za Kathmandu.
Kitovu cha tetemeko hilo inadaiwa kuwa takriban kilomita 83km Mashariki mwa Kathmandu, eneo lililoko karibu na mpaka wa China.
No comments:
Post a Comment