 |
| Eneo ambapo shambulio hilo limefanyika. |
 |
| Migahawa ikiwa imefungwa baada ya tukio hilo kutokea. |
 |
| Polisi akiangalia hali ya usalama katika eneo hilo. |
 |
| Baadhi ya watu waliokamatwa kwa kuhusishwa na shambulio hilo. |
 |
| Watu waliokuwa eneo la mgahawa wa Twin Peak wakijaribu kuondoka ili kuokoa maisha yao. |
 |
| Hali ya usalama katika eneo hilo. |
 |
| Polisi wakizidi kuimarisha ulinzi. |
Polisi nchini Marekani wamesema kuwa
watu tisa wameuawa katika shambulio lililotekelezwa na watu wenye silaha
waliokuwa kwenye pikipiki katika mgahawa wa Twin Peaks uliopo katika
jimbo la Texa mjini Waco jana jumapili majira ya mchana.
Hata hivyo watu wengine 18 walijeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu kutokana shambulio hilo.
Maofisa wa serikali katika mji huo wanasema kuwa, walibaini
mkusanyiko kati ya watu watano walioonekana kupanga jambo lisilo la
kawaida.
Watu waliokuwa katika mgahawa huo walijificha katika chumba cha
majokofu katika harakati za kujiokoa kabla ya kusaidiwa na Polisi kutoka
katika eneo hilo.
PICHA NA DAILY MAIL NEWS
No comments:
Post a Comment