Kanisa Katoliki nchini Burundi limejiondoa katika mchakato mzima wa uchunguzi na uongozi wa aina yoyote katika uchaguzi huo.
Haya yamearifiwa wakati maandamano dhidi muhula wa tatu wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza yanaendelea kufanyika katika mitaa kadhaa ya mji mkuu Bujumbura kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.
Wakati huohuo, Jumuia ya bara ulaya imesimamisha ujumbe wake uliokuwa usimamie uchaguzi mkuu nchini Burundi.
EU inasema kuwa uamuzi huo umeafikiwa kwa sababu ya sheria kali dhidi ya vyombo vya habari, matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji, na mazingara mabaya ya vitisho kwa vyama vya upinzani.
Makundi ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa zaidi ya watu 20 wamefariki wakati wa ghasia za maandamano,
tangu rais Pierre Nkurunziza alipotangaza mwezi uliopita kuwa anapania kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu, kinyume na katiba ya Burundi.
Uchaguzi wa urais umepangiwa kufanyika Juni tarehe tano, huku ule wa urais ukiwa mwishoni mwa mwezi huo wa Juni.
No comments:
Post a Comment