Pages

Thursday, 4 June 2015

Agentina waandamana kutetea wanawake

Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Argentine - Buenos Aires kupinga mateso dhidi ya mwanamke. Maandamano hayo yamefuatia mfulurizo wa visa vya mauaji yaliyoshtua taifa hilo, yakiwemo yale ya mwalimu wa chekechea ambaye bwana yake alimkata koo mbele ya darasa lake.


Vyama vya wafanyakazi , vyama vya kisiasa na kanisa katoliki wameunga mkono maandamano hayo .

Argentina imepitisha sheria dhidi ya unyanyasaji wa nyumbani, lanini wanaharakati wanasema kuwa hazitekelezwi ipasavyo. Maandamano ya watu wachache pia yamefnyika katika nchi jirani za Chile na Uruguay.

No comments:

Post a Comment