| Andy Murray |
Mcheza tenis wa Uingereza Andy
Murray amefanikiwa kumcharaza Jeremy Chardy wa Ufaransa na kutinga hatua
ya robo fainali ya michuano ya French Open ikiwa mara yake ya tano.
Murray,
anayeshika nafasi ya tatu kwa ubora wa wacheza tenisi wanaume duniani,
kwa kuanza kumchapa 6-4 3-6 6-3 6-2 katika mchezo uliodumu kwa saa mbili
na sekunde 51.Sasa atapambana na David Ferrer, anayeshika nafasi ya saba kwa ubora, ambaye alimbwaga Marin Cilic 6-2 6-2 6-4. Cilic anashika nafasi ya tisa kwa viwango vya ubora.
Murray, mwenye umri wa miaka 28, kwa sasa ameshinda michezo yote 14 aliyocheza kwenye viwanja vya udongo kwa mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment