Barua pepe iliopatikana na gazeti
moja la Afrika kusini na kuonekana na BBC inatoa ushahidi zaidi kwamba
aliyekuwa rais wa taifa hilo Thabo Mbeki na rais wa FIFA Sepp Blatter
walikubaliana kuhusu kitita cha dola millioni kumi ambacho maafisa wa
mashtaka nchini Marekani wanasema ilikuwa hongo ya taifa la Afrika
Kusini kupewa maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2010.
Katika
barua hiyo katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke alimuandikia waziri mmoja
wa Afrika Kusini akimtaka kueleza ni lini fedha hizo zitatolewa kwa kuwa
tayari Blatter na Mbeki walijadiliana kuhusu swala hilo.
Serikali ya Afrika Kusini inasisitiza kuwa fedha hizo zilitolewa kihalali kukuza soka katika visiwa vya Carebbean.
SOURCE: BBC
No comments:
Post a Comment