Kiungo Lansana Camara kutoka Sierra
Leone amesema anafurahia mazoezi katika klabu ya Yanga na ana imani
mabingwa hao wa Tanzania Bara watamsajili kwa ajili ya msimu ujao.
“ Nina furahia mazoezi yangu na mashabiki wengi wanakuja kutuangalia, hii inatia moyo”, amesema Camara, amambaye anafanya mazoezi na timu hiyo kwa sasa.
Yanga imeanza mazoezi Jumatatu wiki hii katika viwanja vya kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.
Mashabiki wengi na makocha wa Yanga, Mdachi Hans Pluijm na msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa wanaonekana kuvutiwa na mchezaji huyo mwenye umbo la kuvutia kisoka na wana imani ataisaidia timu hiyo endapo ataonekana anafaa.
No comments:
Post a Comment