| Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, Sospeter Christopher Boyo (aliyesimama mwenye shati la kitenge) akisoma taarifa fupi ya Kambi ya Nyarugusu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (aliyeketi mwenye suti ya kijivu) aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye kambi hiyo kujionea hali halisi ya mazingira na changamoto zinazowakabili Waomba hifadhi wa Burundi na Kongo. |
| Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) huku Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (wa nne kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushoto) mara tu baada ya kuwasili na kusomewa taarifa kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. |
Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa
kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile akifafanua jambo kwa Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe wakati akitembelea na
kukagua maeneo mbalimbali ya Kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu,
mkoani Kigoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa,
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la
Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakikagua sehemu
wanayolala Waomba hifadhi wanaoendelea kuwasili katika kambi ya
Nyarugusu ambayo inaelemewa kutokana na wingi wa Waomba hifadhi hao
wanaoendelea kumiminika mjini Kigoma.
Muonekano wa moja ya chumba cha kulala
familia za waomba hifadhi katika kambi ya Nyarugusu ambapo kifika muda
wa kulala wanatandika mkeka chini katika vumbi hilo jekundu na kupata
usingizi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe (mwenye suti ya kijivu), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez (wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto)
wakisikiliza hoja mbalimbali kutoka kwa Waomba hifadhi wanaohifadhiwa
kwenye kambi ya Wakimbizi Nyarugusu iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani
Kigoma walipotembelea kambi hiyo kukagua kambi hiyo na kuangalia
changamoto mbalimbali zinazowakabili na namna ya kuzitatua.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe (mwenye suti ya kijivu) akiteta jambo na Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez wakati walipotembelea kambi ya Wakimbizi ya
Nyarugusu iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma mwishoni mwa juma
lililopita.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe akigawa vifaa vya matumizi ya nyumbani ambavyo ni
Blangeti, Mkeka, Kontena la kuhifadhi chakula na dumu la maji la lita 10
kwa mmoja wa Waomba hifadhi waliowasili siku ya ziara ya kutembelea
kambi ya Nyarugusu mwishoni mwa juma wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Anayeshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
(mwenye shati jeupe).Kulia ni Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa
kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile.
Waomba hifadhi na familia zoa wakiwa katika foleni ya kupokea vifaa hivyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe akizungumza na Waomba hifadhi katika kambi ya Nyarugusu
wakati alipofanya ziara ya kutembelea eneo hilo akiwa ameambatana na
Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na Mwakilishi wa shirika la
kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR).
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akizungumza na
mmoja wa wakinamama anayeishi kwenye kambi ya Wakimbizi Nyarugusu wakati
wa ziara maalum ya kutembelea maeneo hayo iliyohusisha Serikali ya
Tanzania na Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa
(UN) Tanzania, Hoyce Temu wakibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyakazi
wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M) (katikati) ambaye jina lake
halikuweza kupatikana kiurahisi katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu
iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za
Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (mwenye
suti ya kijivu) akifafanua jambo kwa Mh. Mathias Chikawe alipotembela
katika chumba maalum kichotumika kufanya usajili kwa Waomba hifadhi na
familia zao kwa ajili ya kupewa hati ya kuwa Wakimbizi kamili kama
watatimiza vigezo vinavyohitajika. Aliyeketi kulia ni Msajili wa Waomba
hifadhi, Ndalo Charles Bogohe.
Zoezi la usajili likiendelea kwa familia za waomba hifadhi katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Akinamama wakiandaa chakula cha mchana kwa familia zao.
Sehemu ya familia za Waomba hifadhi
katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Geita
wakiendelea kujipanga baada ya kuwasili kwenye eneo hilo.
Moja ya familia za waomba hifadhi ikiwa
imejipumzisha mara baada ya chakula cha mchana huku nyuso zao
zikionekana kuwa na furaha na matumaini mapya.
Hili ni eneo ambalo Waomba hifadhi kutoka nchini Burundi wa kambi ya Nyarugusu wakiteka maji safi kwa matumizi yao.
Harrison Mseke (kushoto) akizungumza
jambo na Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) wakati wakielekea kukagua
vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Mapendo ambayo yamegeuzwa
kuwa nyumba za kulala Waomba hifadhi, kutokana na uhaba wa makazi ya
kuishi kwenye maeneo ya kambi ya Nyarugusu. Wengine pichani ni baadhi ya
viongozi wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika
msafara huo.
Baadhi ya Waomba hifadhi katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu wakiwa wamempumzika huku wengine wakipata chakula cha mchana.
Kinababa nao hushiriki kuandaa chakula cha mchana kwa familia zao.
Eneo la shule ya msingi Mapendo katika
kambi ya Wakimbizi Nyarugusu ambalo kwa sasa linatumika kuhifadhi Waomba
hifadhi wanaoendelea kuwasili nchini wakitokea Burundi kupitia mji wa
Kigoma.
Madawati ya wanafunzi katika shule ya
msingi Mapendo yakiwa nje ya madarasa yakitumika kuanikiwa nguo na huku
wakati wa msimu wa mvua yakinyeshewa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
wakibadilishana mawazo na wasimizi wa kambi hizo za Nyarugusu wakati wa
ziara ya siku moja wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Alvaro Rodriguez (kushoto) akiwa
ameambatana na Mh. Chikawe wakikagua eneo jipya litakaloitwa Nyarugusu B
lililotolewa na serikali kwa ajili ya Waomba hifadhi wanaoendelea
kumiminika mjini Kigoma ambalo liko mbioni kutengenezwa na kukamilika
ndani ya miezi 3 ijayo.
Eneo jipya la kambi ya Nyarugusu B ambalo
limetengwa na serikali ya Jamhuri ya Tanzania kwa ajili ya makazi ya
Waomba hifadhi wanataotenganishwa Burundi na Congo mara tu baada ya
kukamilika.
Muonekano wa eneo jingine la makazi ya Waombahifadhi ndani ya kambi ya Wakimbizi Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu.
Amani na upendo itawale kati
yetu......ndivyo wanavyosema kwa pamoja baadhi ya watoto waomba hifadhi
wakifurahia picha pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
WAKATI dunia kupitia
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanahangika kutanzua changamoto za
wakimbizi Nyarugusu, mkoani Kigoma imeelezwa kuwa idadi kubwa ya
Wakimbizi waliorejeshwa nchini Burundi kutoka kambi ya Mtabila iliyoko
Kigoma iliyofungwa rasmi Desemba, 2012 wameingia tena nchini na kujazana
katika makazi ya muda ya Nyarugusu wakiomba hifadhi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kambi ya
Nyarugusu Sospter Christopher wakati akizungumza na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi aliyekwenda kuangalia hali halisi ya kambi ya Nyarugusu na
Wakimbizi akiambatana na Maofisa wa Umoja wa Mataifa akiwemo Mratibu wa
Mashirika hayo nchini Alvaro Rodriguez.
Kurejea kwa wingi kwa Wakimbizi hao ni pigo
kisaikolojia kwa watu ambao walirejeshwa nyumbani kwa kuonekana kwamba
hali ni shwari na walikuwa wameanza kuishi maisha ya kawaida.
Mkuu huyo wa kambi alisema idadi hiyo
ikichanganyika na wengine imafanya kambi kuhemewa na kuonekana haja ya
kutafuta eneo jingine la kupiga kambi kwa ajili ya Wakimbizi hao ambao
mpaka mwishoni mwa wiki iliyopita walikuwa zaidi ya elfu 51.
“ Kwa sababu tunapokea idadi kubwa ya
waomba hifadhi toka Burundi, tumekuwa tukiongeza idadi ya vituo vya
mapokezi ili kukidhi mahitaji ya kuwapokea wakati tukisubiri maelekezo
toka ngazi za juu za kuwahamishia Migunga Hills eneo linalopendekezwa
kufunguliwa kambi ya Nyarugusu B” alisema Christopher mbele ya Waziri
Chikawe.
Alisema walianza kupokea waomba hifadhi
hapo kambini kuanzia Aprili 29, 2015 kwa idadi ndogo kabisa ya watu 36,
lakini idadi hiyo ilianza kuongezeka siku hadi siku na kufikia Mei 27
mwaka huu idadi yao ilifikia 48,333, idadi kubwa ikiwa wanawake na
watoto.
Wakimbizi hao walikuwa wakipitia vituo vya Kigoma (27,638), Manyovu (4,439), Kilelema (1,603) na Kigadye (1,291).
Kambi hiyo yenye uwezo wa kubeba watu
50,000 imeelemewa kwa sababu ya ujio mpya uliosababisha kuwepo kwa
Wakimbizi zaidi ya 106,410.
Kuna matatizo zaidi ya milipuko ya wagonjwa
kambi hii imechanganywa na Wakimbizi wa Kongo watu ambao hawana
utamaduni wa pamoja na kuonekana hatari ya kukabiliana kwa
kutosikilizana.
Aidha kambi hiyo pamoja na kuwahifadhi
waburundi wapo pia Wakimbizi kutoka Kongo wapatao 54,706; Burundi,3261 ;
Rwanda 72; Uganda 17; Sudan Kusini wanane; Kenya 7; Somalia 3; Ethiopia
1; Zimbabwe 1; na Ivory coast 1.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari
walioambatana naye katika ziara hiyo kuhusu hali ya baadae ya Wakimbizi
wa Kongo ambao wapo nchini kwa takribani miaka 19 sasa, Waziri Chikawe
alisema kwamba serikali haina mpango wa kuwapa uraia kwa sasa ingawa
Marekani imesema itawachukua Wakimbizi elfu 30 kuwapeleka kwao na
kwingine duniani.
“hatuna mpango wa kuwapa uraia kwa sasa…”
alisema Chikawe na kusema kwamba kwa kuondolewa kwa hao wengine
kutasaidia kupunguza idadi yao katika kambi hiyo.
Alisema kwamba ni lengo la serikali
kuhakikisha kwamba kambi hiyo inapunguzwa ili kuweza kuchangia ipasavyo
kwa hali bora ya Wakimbizi na kwamba mchakato wa kuwaangalia waomba
hifadhi kama wanafaa kuwa Wakimbizi unaendelea.
Akizungumzia malalamiko ya upatikanaji wa
chakula, Waziri Chikawe alisema kwamba si kweli kuwa kuna watu
hawajapata chakula kwa siku saba la sivyo wangelikufa.
Alisema wengi wa Wakimbizi ni watoto na
kwamba wanapoingia nchini wanapewa vyakula vikavu (kama biskuti) lakini
wakishafika kambini wanapewa chakula kilichopikwa na resheni ya siku 14 .
Alisisitiza kuwa kama kungelikuwa hakuna chakula watoto hao wasingeishi, labda kama wanataka kuongezewa chakula zaidi.
Kuhusu ujenzi wa kambi mpya Migunga alisema
kwamba wataalamu wanaangalia barabara mbadala kwani iliyopo sasa pamoja
na kuhitajika milioni 300 kuitengeneza lakini bado kila mvua
itakapokuwa inanyesha itahitaji kutengenezwa.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole katika mahojiano
na waandishi wa habari aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kufungua
mipaka ili Wakimbizi waweze kuingia na kutoa eneo kwa ajili ya kambi
mpya kutokana na ya sasa kujaa sana.
Aidha aliishukuru serikali ya Uingereza kwa
kuwa ya kwanza kutoa misaada kwa ajili ya Wakimbizi hao na kutarajia
nchi nyingine kama Marekani itafanya hivyo mapema ili kuisaidia serikali
ya Tanzania katika kuhudumia waomba hifadhi.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez amesema wanafanya kila linalowezekana
ili kupunguza idadi ya Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu kwa kuwapatia
eneo jingine la kujihifadhi.
Alisema kwa kuwatoa hapo watasaidia shule
zilizofungwa ambazo zinasomesha watoto kutoka kwa Wakimbizi wa Kongo
kurejea madarasani kukamilisha mtaala wao.
(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
No comments:
Post a Comment