Barua inayosemekana iliandikwa na
rais wa shirikisho la soka nchini Afrika kusini, Danny Jordaan,
inaonekana kuongeza uzito kwenye shutuma kwamba serikali ya nchi hiyo
ilificha malipo ya pesa kiasi cha dola milioni kumi kwa FIFA .
Inasema kuwa kufuatia mazungumzo na waziri wa mambo ya nje Bwana Jordaan aliomba pesa hizo zilipwe kwa njia zisizo za moja kwa moja.
Maafisa wa Afrika Kusini wamesisitiza kuwa pesa hizo hazikuwa za rushwa kwa ajili ya kupokea mashindano ya fainali ya kombe la dunia la mwaka 2010.
Wanasema yalikua ni malipo halali kuunga mkono maendeleo ya soka katika nchi za Caribbean
No comments:
Post a Comment