Idadi kubwa ya ndovu yatoweka Tanzania
Wanaharakati wa wanyamapori
wameelezea hali ya kutoweka kwa idadi ya ndovu kwa asilimia sitini
nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kama janga.
Kundi linalofuatilia maisha ya wanyamapori, TRAFFIC, linasema idadi hiyo inaashiria kiwango halisi cha uwindaji haramu.
Waziri
katika serikali ya Tanzania Lazaro Nyalandu, amesema kuwa tatizo hilo
lipo kwa kiwango tofauti nchini humo, akitoa mfano kuwa eneo la
Serengeti idadi yao inaongezeka . Amesema mamia ya walinzi wa wanyamapori wamekodiwa kukabiliana na uwindaji haramu
No comments:
Post a Comment