Aliyekuwa makamu wa rais wa
shirikisho la Soka Duniani FIFA, Jack Warner, ameituhumu Marekani kwamba
inafuatilia mashtaka ya rushwa dhidi ya maafisa waandamizi wa shirika
hilo kwa sababu imeshindwa kuwa mwenyeji wa kombe la dunia la mwaka
2022.
| Jack Warner |
Warner amekana tuhuma hizo. Shirikisho hilo la Soka Duniani limegubikwa na tuhuma za rushwa kwa kipindi cha wiki mbili mfululizo. Akiandika katika gazeti lake linaloitwa Sunshine, Warner anaelezea mashtaka ya Marekani dhidi yake kuwa ni uonevu na yaliyoegemea upande mmoja.
Katika makala yake, Warner ameendelea kujitetea kwa kusema kuwa, kuishutumu Afrika Kusini kunachafua hadhi ya hayati Nelson Mandela ambaye ameisaidia Afrika Kusini kupata nafasi hiyo.
Gazeti hilo limeonyesha picha za Jack Warner akikutana na Prince William, David Beckham, Barack Obama na Vladimir Putin ambao amesema wote walikuwa na ushawishi pindi nchi zao zilipokuwa zikifanya kampeni ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia.Jack Warner amemalizia kwa kuuliza iwapo walikuwa wanatumia takrima kama rushwa?
Jack Warner ni mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa bodi ya shirikisho la soka duniani FIFA, ambao wanatuhumiwa kwa kashfa ya rushwa na mpaka sasa Warner amekana tuhuma zote zinazomkabili.
No comments:
Post a Comment