Makamu wa Rais wa zamani wa
Shirikisho la Kandanda duniani FIFA Jack Warner amekumbwa na kashfa
ingine na uchunguzi dhidi yake kuhusiana na kupotea kwa fedha ambazo
zililengwa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi
lililoikumba Haiti mwaka 2010.
Lakini hata hivyo, Wachunguzi wa kashfa hiyo rushwa inayoikabili FIFA wanasema fedha hizo zilihamishwa katika Akaunti inayodhibitiwa na Bwana Warner kwa ajili ya matumizi yake binafsi. Miaka minne baadaye fedha hizo bado hazijatolewa maelezo.Warner mwenyewe amekana tuhuma zote zilizotolewa dhidi yake.
No comments:
Post a Comment