Waziri mkuu wa zamani Mh.Edward Lowasa aliyeko kanda ya ziwa kutafuta
wadhamini amepata wakati mgumu alipowasili mkoani Mara baada ya makundi
ya wananchi wakiwemo vijana, wanawake na watoto kumfuata kila
alikokwenda wakitaka wapewe nafasi ya kumueleza kero zao jambo
lililosababisha zoezi la kumdhamini kuwa gumu licha ya kufanikiwa kwa
kiasi kikubwa.
Heka heka za wananchi kutaka kuzuia msafara wa Mh.Lowasa zilianza mapema
asubuhi wakati anawasili kwenye uwanja wa ndege wa musoma ambapo
vijana walizuia msafara wake kutoka kwenye uwanja huo wakitaka wapewe
nafasi ya kuonana naye.
Baada ya waratibu wa msafara huo kufanya kazi ya ziada ya kufanikiwa
kutatua changamoto hiyo Mh.Lowasa aliekea katika wilaya ya Bunda na
licha ya kusimamishwa na wananchi njiani hali ilikuwa ngumu zaidi
katika ofisi ya CCM wilaya ya hiyo kutokana na watu kujitokeza kwa
wingi.
Hata hivyo pamoja na maelfu ya wananchi hao wanaounga mkono safari ya
matumaiani kuwa na shauku ya kumueleza Mh.Lowasa shida zao alishindwa
kuwasikiliza kutokana na kubanwa na kanuni na aliwaomba kuwa watulivu
na kuendelea kuiombea kheri safari ya matumaini.
Mh.Lowasa akiwa katika mkoa wa Mara amepata idadi kubwa ya wadhaamini
pia amefika nyumbani kwa hayati baba wa taifa Mwalimu Nyerere na kupewa
baraka, kisha kuweka shada la maua kwenye kaburi na pia ametembelea
wilaya ya Tarime na Musoma.
Mh.Lowassa ambaye ameshatembelea mikoa ya Mwanza Geita,Zanzibar na Pemba
anaendelea na ziara yake ya kutafuta wadhamini katika mkoa wa Simiyu.
Maelfu ya Wananchi wakiwa wameuzuia Msafara wa Lowassa
wakishinikiza kumuona, hali iliyowalazimu Polisi na waratibu wa
msafara ya kutumia njia mbadala kutatua changamoto hiyo
Mh. Lowassa alipotembelea Kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwl. J.K. Nyerere

No comments:
Post a Comment