MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Athuman
Machuppa, ameiangalia Ligi Kuu Bara msimu wa 2014-2015 uliomalizika
mwishoni mwa wiki na kutoa yake ya moyoni.
“Viwanja ni tatizo, hatuwezi kuona ubora wa
wachezaji wenye vipaji kama viwanja ni bomu ni Tanzania pekee zaidi ya
mechi tano zinalazwa viporo na kuchezwa kwa siku mbili, hili ni lazima
TFF ilibadilishe soka ni viwanja vipaji vinaonekana kwenye uwanja nzuri.
“Hata sisi mafanikio ya mwaka 2003 yalianzia
kukusanywa tangu mwaka 1999 kwa vile tulipokewa vema na wazoefu
tuliowakuta na kutunzwa vema kwa miaka mitatu na kuja kuwa tishio ndani
na nje ya nchi, hata Simba ya sasa inapaswa kupewa muda ina vijana wenye
vipaji.
“Kikosi kisipanguliwe, penye mapungufu paboreshwe
na vijana wasiyumbishwe kwa kubadilishiwa makocha kila mara, wastani wa
miaka 23 walionao wachezaji ni msaada mkubwa kwa Simba kuja kutetemesha
Afrika mbele ya safari, vijana wana vipaji sana.”
Machuppa anayeishi Sweden alikokuwa akicheza soka
la kulipwa, alizikumbusha pia klabu za soka nchini akisema: “Wazawa
wathaminiwe kama wanavyothaminiwa wageni, itasaidia kujenga umoja ndani
ya timu, ubaguzi unaofanywa kwa kuwathamini wageni na kuwapuuza wazawa
wenye mchango mkubwa katika timu ni tatizo.
“Nazipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa na Azam kwa
kushika nafasi ya pili, nazikumbusha kufanya maandalizi mapema kwani
tiketi za kimataifa wanazo, hivyo wasilaze damu kisha kuja kutuaibisha
mwakani, zijipange zicheze hatua ya makundi,” alisema.
Ligi ya Bara ilimalizika Jumamosi Yanga
ikitangazwa mabingwa kwa kukusanya pointi 55, kisha kufuatiwa na Azam
wenye pointi 49 na Simba wakishika nafasi ya tatu kwa pointi 47, huku
Polisi Moro na Ruvu Shooting zikishuka daraja.
No comments:
Post a Comment