Serikali ya marekani yakumbwa na
udukuzi mtandao wa komputa ambapo taarifa binafsi za mamilioini ya
wafanyakazi wa serikali zimeingiliwa. Ofisi ya Utumishi ya nchini
hiyo inasema karibu ya watu milioni nne ambao wanafanya kazi au waliwahi
kufanya kazi wameathirika na udakuzi huo.
Idara ya Utumishi ya
Serikali ya Marekani inayosimamisha huduma za wafanyakazi wa umma nchini
huo imefanya uchunguzi wa usalama wa taarifa za wafanyakazi wake
wapatao milioni nne.
Idara hiyo inasema wadakuzi hao walililenga
kuingilia taarifa hizo kwa njia ya mtandao tangu mwezi aprili jambo
linalofanyiwa uchunguzi na shirika la kijasusi la FBI.
Taarifa
zote za udakuzi huo na idadi ya watu waliohusika bado haijafahamika
lakini Afisa mmoja anasema kila idara ya serikali itakuwa imeathirika
kwa kiasi kikubwa.
Mjumbe wa Kamati ya kiintelejensia ya Baraza la Seneti imewalamu wadakuzi kutoka nchini China kuhusika na udakuzi huo.
Hii sio mara ya kwanza kwa taarifa muhimu kama kama hizo kufanyiwa udakuzi.
Mwezi
Machi mwaka jana,wadakuzi walijaribu kufanya udakuzi kwa wafanyakazi wa
serikalini ambapo pia mwezi Novemba taarifa za za wafanyakazi wa Wizara
ya Mambo ya ndani wapatao elfu ishirini zilidakuliwa.
No comments:
Post a Comment