Uchaguzi wa ubunge wafanyika Uturuki
Uturuki inandaa uchaguzi wake wa
ubunge leo jumapili. Matokeo ya kura hiyo yataamua ikiwa chama tawala
cha AK cha rais Recep Tayyip Erdogan kitapa ushindi wa kukiwezesha
kuifanyiamabadiliko katiba na kuifanya Uturuki kuwa nchi inayongozwa na
rais.
AK kimeshinda kila uchaguzi tangu mwaka 2012 lakini bwana
Erdogan amekuwa akilaumiwa kufuatia uongozi wake unaofananishwa na wa
kiimla. Ikiwa chama cha HDP kitapata zaidi ya asilimia 10 na
kuingia bungeni kwa mara ya kwanza kitainyima serikali theluthi mbili ya
viti inavyohitaji.
No comments:
Post a Comment