Ugiriki imetangaza kuchelewa kulipa
deni la Euro milioni mia tatu ambalo walitakiwa kulilipa shirika la
kimataifa la fedha la IMF siku ya Ijumaa.
Serikali ya Ugiriki
imesema itachanganya kwa pamoja malipo hayo ambayo yalikuwa yalipwe kwa
mafungu manne mwezi June ya kuyalipa kwa pamoja mwishoni mwa mwezi huu.
Utaratibu huo ambao unaruhusiwa na kanuni za IMF,uliwahi kufanywa na nchi ya Zambia miongo mitatu iliyopita. Mwandishi
wa BBC wa masuala ya uchumi anasema mpango huo unaweza kuwa mbinu
ambayo Ugiriki umeitumia ili kuweka msisitizo kwa wadeni wake wa
kimataifa wakati huu nchi hiyo ikitafuta ufumbuzi wa madeni
yanayolikumba taifa hilo.
No comments:
Post a Comment