Umoja wa Mataifa unasema kuwa serikali ya Eritrea inaendesha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya watu wa nchi hiyo.
Imesema kuwa hali hiyo imesababisha maelfu ya watu kuihama nchi hiyo. Eritrea inachukua nafasi ya pili baada ya Syria kuwa nchi wanakotoka wahamiaji wengi wanaojaribu kuvuka bahari ya Maditerranean.
Ripoti hiyo inasema kuwa dhuluma zikiwemo mauaji ya kiholela, kukamwata kwa watu, mateso na kazi za lazima ni baadhi ya yale yanayoendelea nchini Eritrea.
No comments:
Post a Comment