Mhandisi
wa Mazingira wa Mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa
mazingira(NEMC)Arnold Kasilaga.akiongea na wafanyakazi wa Vodacom
Tanzania na wafanyakazi wa Mlimani City.Wakati wa kuadhimisha siku ya
mazingira duniani ambapo wafanyakazi hao walifanya kazi ya usafi kwa
vitendo kuzunguka maeneo ya Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Kitengo cha Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania Karen
Lwakatare,akiongea jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na
wafanyakazi wa Mlimani City.Wakati wa kuadhimisha siku ya mazingira
duniani ambapo wafanyakazi hao walifanya kazi ya usafi kwa
vitendokuzunguka maeneo ya Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Mhandisi
wa Mazingira wa Mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa
mazingira(NEMC)Arnold Kasilaga(kushoto)na Mkuu wa Kitengo cha Afya na
Usalama wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare(katikati)wakimsikiliza jambo
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Rosalynn
Mworia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya mazingira duniani
ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na wafanyakazi wa
Mlimani City walifanya kazi ya usafi kwa vitendo kuzunguka maeneo ya
Mlimani city jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku hiyo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na wafanyakazi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakifanya usafi wa mazingira
kuzunguka maeneo yanayozunguka ofisi zao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha
siku ya mazingira duniani.
Mkuu
wa Kitengo cha Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania Karen
Lwakatare,akiweka uchafu katika moja ya vyombo maalum vya kuhifadhia
uchafu baada ya kukusanya uchafu wakati wa kuadhimisha siku ya mazingira
duniani ambapo wafanyakazi kampuni hiyo na pamoja na wafanyakazi wa
Mlimani City walifanya kazi ya usafi kwa vitendokuzunguka maeneo ya
Mlimani city jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku hiyo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wafanyakazi wa Mlimani city
wakimsikiliza Mhandisi wa Mazingira wa Mamlaka ya udhibiti na usimamizi
wa mazingira(NEMC)Arnold Kasilaga(hayupo pichani)wakati wa hafla fupi ya
siku ya mazingira duniani ambapo wafanyakazi hao walifanya kazi ya
usafi kwa vitendo kuzunguka maeneo ya Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Juni 5,2015:Mhandisi wa Mazingira kutoka Mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa mazingira (NEMC) Bw.Arnold Kasilaga,amesema jukumu la utunzaji mazingira ni la kila mmoja kwa kuwa shughuli mbalimbali zinazofanywa na binadamu zinachangia kuharibu mazingira.
Bwana Kasilaga aliyasema hayo leo wakati akiongea na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na Mlimani City ambao wameshirikiana katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani kwa kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka ofisi zao ikiwemo viwanja vya eneo maarufu la biashara na Mikutano ya Kimataifa la Mlimani City."Utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila moja hivyo hakikisheni katika shughuli zetu mnazofanya mnatanguliza suala la utunzaji mazingira ama sivyo athari mbalimbali zinazotokana na uharibifu wa mazingira zitakuwa zikiendelea kujitokeza kila siku"Alisema
Wafanyakazi hao wametumia muda wao kushiriki katika kufagia mazingira,kupanda miti,kusafisha mitaro ya maji machafu na kufyeka nyasi ili kuweka mazingira kwenye hali ya usafi.
Mkuu wa kitengo cha Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare,amesema kampuni ya Vodacom imekuwa mstari wa mbele kuhamasisha utunzaji wa mazingira na ndio maana inaipa umuhimu mkubwa siku ya leo ambayo ni siku ya Mazingira Duniani.
“Kwetu Vodacom siku ya leo ni muhimu sana kwa maana tunaamini kuwa utunzaji wa mazingira ni suala muhimu sana katika dunia ya leo na ndio maana tumeamua kuiadhimisha kwa vitendo ambapo wafanyakazi wetu wametumia muda wao kushiriki kazi za usafi,upandaji miti na kutoa elimu ya umuhimu wa kutunza mazingira kwenye vikundi mbalimbali vya jamii”.
Shirika la Umoja wa Mataifa linaoshughulika na mazingira (UNEP) limetangaza tarehe 6 ya mwezi Juni kama Siku ya Mazingira duniani ambapo huadhimishwa kaika nchi mbalimbali duniani kwa kuhimiza utunzaji wa mazingira ambapo makundi mbalimbali hushiriki katika masuala ya kusafisha mazingira na kupanda miti.
Kauli mbiu ya siku ya mazingira Duniani kwa mwaka huu ni Ndoto bilioni saba.Dunia moja.Tumia raslimali kwa uangalifu ambayo inatoa ujumbe kwa kila mmoja anayeishi duniani kuzingatia utunzaji wa mazingira katika kila jambo analofanya.
Kwa hapa nchini maadhimisho haya ya Wiki ya Mazingira ambayo imefikia kilele leo yalizinduliwa rasmi mapema wiki hii na maonyesho ya shughuli za utunzaji mazingira yamefanyika sehemu mbalimbali nchini na mkoani Tanga ambapo yanaadhimishwa kitaifa.
No comments:
Post a Comment