Pages

Friday, 5 June 2015

WIKI YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA


 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati), akikabidhi kikombe kwa mfanyakazi wa kampuni ya Green WastePro Ltd kwa mchango wao mkubwa katika kutunza wa mazingira.

 
Wawakilishi wa makampuni na taasisi wakipokea vyeti na medali kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto), aliyekuwa mgeni rasmi.

 
Medali na vyeti vikitolewa.

 

Sehemu ya wanananchi waliohudhuria hafla hiyo.

 

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mirambo ya Manispaa ya Kinondoni Dar waliohudhuria maadhimisho hayo.  Kulia ni  walimu wao.

 
...Wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi zao za ushindi uliotokana na utoaji elimu juu ya usafi wa mazingira.

 

Wafanyakazi wa Kampuni ya Green WastePro Ltd wakiwa na medali yao.

 
Mwanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Ualimu (DUCE) tawi la UDSM Chang'ombe, Temeke,  Dar,   akipokea zawadi ya kombe na cheti kwa mchango wao wa uboreshaji wa mazingira.

 
Gari la Kampuni ya Green WastePro Ltd linalotumika kubeba uchafu.

 
Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira na Naibu Meya Wilaya ya Kinondoni, Richard Chengula (kushoto) akizungumza jambo.  Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati).

 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati), akiwa na baadhi ya wananchi waliopata zawadi za kwa usafi wa usafi wa mazingira.
WILAYA ya Ilala ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Raymond Mushi,  leo imeongoza wiki ya maadhimisho ya Mazingira katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.
Mushi ambaye ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi katika wiki ya maadhimisho hayo ametoa vyeti na medali kwa baadhi ya shule za msingi na sekondari, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali kutokana na mchango walioutoa katika uboreshaji wa mazingira hapa nchini.
Alisema kuwa licha ya taasisi hizo kujitahidi katika kuhakikisha mazingira yanakuwa katika sehemu safi,  pia kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa  chachu ya uchafuzi wa mazingira ikiwemo kuchimba mchanga sehemu isiyotakiwa na kusababisha mazingira kuendelea kuwa machafu, hivyo aliwataka kuacha.
“Taasisi pamoja na makampuni mengi yamejitahidi sana kurekebisha mazingira kwa kuyaweka katika hali safi lakini kuna baadhi ya watu amabao wamekuwa chanzo cha kuchafua mazingira hasa kwa wachimbaji wa mchanga sehemu isiyotakiwa hivyo nawaomba kuacha ili kutoendeleza kuchafua mazingira,”  alisema.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira na Kaimu  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Richard Chengula, aliitaja Ilala kuwa ni wilaya inayoongoza kwa kutilia maanani mazingira, na hivyo akazitaka wilaya zingine kuongeza bidii ya kutunza.
Maadhimisho hayo leo yameambatana na utoaji wa vyeti, medali, vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kwa makampuni, mashule, mabenki na vyuo.
Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa mkoani Tanga huku kauli mbiu yake ikiwa ni “Ndoto bilioni saba, dunia moja.Tumia rasilimalimali kwa uangalifu”.
NA DENIS MTIMA/GPL

No comments:

Post a Comment